AfyaHabari

Maafisa wa usalama eneo la taveta kaunti ya Taita taveta wamewakamata wanaharakati 11 wa kutetea haki za binadam waliotaka kuandamana kuhusu mzozo wa afya ambao umekumba kaunti hiyo.

Wakiongozwa na Francis Auma wa shirika la Muhuri, wanaharakati hao wamekamatwa walipokuwa katika harakati za kuanza mandamano hadi ofisi za gavana kulalamikia kudorora kwa afya.

Maafisa wa afya kaunti hiyo wamekuwa katika mgomo kwa muda wa miezi 3 sasa.