AfyaHabari

Serikali ya kaunti ya Tana River imepeleka wahuduma wa afya watano jijini Nairobi ili kupata mafunzo kuhusu chanjo ya covid-19.

Waziri wa afya kaunti hiyo Javan Bonaya amesema hatua hiyo ni njia moja ya serikali ya kaunti kujitayarisha kupokea chanjo hiyo iliyowasiliswa humu nchini hapo jana.

Bonaya amesema wahudumu wa afya na viongozi wakuu wa serikali ya kaunti watapewa kipau mbele kupokea chanjo hiyo.

Vile vile waziri bonaya amesema msajili wa afya na afisa wa ICT watapokea mafunzo hayo ili kuhakikisha wote wanaopata chanjo hiyo watawekwa kwenye sajili itakayosaidia serikali ya kaunti kujua idadi kamili ya watu watakaopokea chanjo hiyo.