AfyaHabari

Kanisa katoliki latangaza kuunga mkono chanjo ya COVID 19….

Kanisa Katoliki linasema kuwa linaunga mkono chanjo ya COVID-19 kwa Wakenya baada ya kuwasili kwa zaidi ya dozi milioni moja za chanjo ya AstraZeneca hapa nchini.

Kulingana na Askofu Mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Nyeri Anthony Muheria, chanjo hio itasaidia pakubwa  kupambana na virusi vya corona  ambavyo vimeathiri pakubwa wakenya huku akipuuzilia mbali msimamo wa muungano wa wa madaktari wa kanisa katoliki kusema kwamba chanjo hio sio salama.

Haya yanajiri siku moja baada ya muungano wa Madaktari wakatoliki nchini Kenya kutoa onyo la ushauri kwa Wakenya dhidi ya kushiriki katika zoezi la chanjo hio.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa muungano huo Stephen Karanja chanjo hio ingestahili kuwachanja wananchi wa wataifa ambayo yameathirika pakubwa na janga hilo kwa angalau mwaka mmoja.