AfyaHabari

Vituo vingi vya karantini vyafungwa kilifi……..

Huku visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vikiendelea kuripotiwa kote nchini imebainika kuwa vituo vingi vya karantini kaunti ya Kilifi vimefungwa.

Kulingana na afisa anayesimamia ugonjwa wa Corona kaunti ya Kilifi Erick Maitha wagonjwa ambao wanapatikana na virusi vya Corona wanajitenga majumbani mwao.

Afisa huyo anasema kituo ambacho kinatumiwa kuwatenga wagonjwa hao kiko eneo la Gede na kile cha Kambi ya Waya.

Wakati huo huo afisa huyo amesema licha ya visa vya maamumbukizi ya Corona kuendelea kupunguka kaunti ya Kilifi haimanisha kuwa Corona imeisha kaunti ya Kilifi.

Maitha amesema mgomo wa wauguzi huenda ukawa ulichangiwa watu wengi kuwa hawajitokezi kupimwa virusi hivyo baada ya kukaa majumbani.