HabariSiasa

Rashid Echesa ni jambazi sugu anayesakwa na polisi…

Aliyekuwa waziri wa michezo na mwanasiasa Rashid Echesa ni jambazi sugu anayesakwa na maafisa wa polisi,haya ni kulingana na inspekta generali wa polisi Hillary Mutyambai.

Hii ni baada ya makataa aliyopewa kujisalimisha kwa polisi kufikia saa saba adhuhuri hii leo kukamilika.

Haya yanajiri huku waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi akiituhumu idara ya mahakama kwa kuwaachilia wanasiasa wanaozua vurugu kwa dhamana.

Anasema juhudi za kuwakabili wanasiasa hao zimelemazwa na idara hiyo ya mahakama.