HabariSiasa

RUTO asema yeye ndiye anayefaa kuwa rais wa taifa hili…

Naibu rais William Ruto kwa mara nyingine tena amemtaka rais Uhuru Kenyatta kumpatia nafasi ya kuendeleza kazi waliyoianza pamoja katika uchaguzi mkuu unaokuja.

 

Ruto ambaye yuko kaunti ya Meru kwa ziara ya siku tatu, amehoji kwamba yeye ndiye bora kuliko wawaniaji wengine wa urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

 

Hata hivyo ameendelea na shinikizo zake za kutafutia umaarufu vuguvugu la hasla nation huku akiwaahidi wakaazi wa eneo hilo kuwaimarisha kiuchumi iwapo watampatia nafasi ya kuwa rais wa taifa hili.