Mbunge wa mvita Abdhulswamad Shariff Nassir Anasema mswada wa marekebisho ya katiba haufai kupingwa katika bunge la kitaifa baada ya kupata uungwaji mkono katika mabunge ya Kaunti.
Katika mahojiano ya kipekee na meza yetu ya habari, Abdhulswamad amesema BBI ina manufaa mengi kwa kila mwananchi na wanaopinga wananjama fiche.
Mbunge huyo anasema viongozi wa siasa wanaopinga ripoti ya BBI wanafaa kuwa wazi na kueleza kwa nini wanapinga ripoti hiyo ili wakenya kuwa na ufahamu.
Kuhusu swala ya ruzuku ya magari ya wawakilish wadi, Abdhulswamad amesema hilo lilikuwa kabla ya mpango huo wa BBI ambao kwa sasa umewasilishwa katika bunge la kitaifa.
Wakati huo huo mmoja wa wanaharakati wa siasa Mjini Mombasa BI hamisa Zaja anadai huenda wabunge pia wakaitisha kiinua mgongo kama ilivyfanyika kwa wawakilishi wadi ili kupitisha ripoti hiyo.