HabariSiasa

Mwashetani atilia shaka baadhi ya vipengee vya BBI…

Mbunge wa Lungalunga kaunti ya Kwale Khatib Mwashetani ametilia shaka baadhi ya vipengee vya mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI.

Mwashetani amesema kuwa gharama ya bajeti ya nchi itapanda endapo idadi ya maeneo bunge na mgao wa serikali za kaunti utaongezwa.

Mwashetani aliyekuwa akizungumza katika eneo la Msambweni, amewataka wananchi kufanya maamuzi ya busara kuhusu mapendekezo ya ripoti ya BBI.

Aidha, Mwashetani amesema kuwa utekelezaji wa ripoti hiyo hasa nyongeza ya mgao wa kaunti kutoka asilimia 15 hadi 35 italiingiza taifa la Kenya katika madeni.

Hata hivyo, kiongozi huyo amependekeza kutekelezwa kikamilifu kwa ajenda nne kuu za miradi ya maendeleo ili kuongeza mapato ya serikali.