AfyaHabari

Raila alazwa katika hospitali ya Nairobi akisubiri matokeo ya covid 19

Oburu Odinga ameondoa wasiwasi kuhusu hali ya afya ya kinara wa ODM Raila Odinga akisema amelazwa katika hospitali ya Nairobi akiwa na machofu mengi ikiwemo kuumwa na mwili.

Oburu anasema wanasubiri matokeo ya vipimo vya covid 19 alivyofanyiwa jana jioni.

Raila amekuwa akilalamikia machofu tangu alipokamilisha ziara ya siku tano ukanda wa Pwani ambapo madaktari walimshauri ajitenge na kupumzika kwa muda wa siku 14.

Haya yanajajiri huku rais wa Tanzania John Magufuli akidaiwa kulazwa katika hospitali ya Nairobi baada ya kuambukizwa virusi vya covid 19 licha ya serikali yake kusalia kimya kuhusiana na alipo rais huyo hta baada ya viongozi wa upinzani nchini humo kuzungumzia hilo.

Duru zimearifu kwamba Magufuli ambayo amekuwa akipinga uwepo wa corona katika mataifa ya Afrika Mashariki anadaiwa kusafirishwa jijini Nairobi siku ya jumatatu baada ya hali yake kuzidi kudhoofika.

Viongozi wakuu wa upinzani nchini humo wanadai kuwa Magufuli amewekwa katika msaada ya kupumua.

Hapo jana Tundu Lissu ambaye aliwania wadhfa wa urais na kushindwa katika uchaguzi wa mwaka jana alikuwa kiongozi wa kwanza kuuliza maswali kuhusiana na alipo rais huyo.