HabariMakalaMazingiraMombasa

Mabaharia waitaka KMA iwape ruzuku ya masomo…

Muungano wa mabaharia nchini unaitaka mamlaka ya ubaharia KMA kuwapa ruzuku ya masomo ambayo hutolewa kila mwaka ili kufadhili mafunzo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa muungano huo captain Haransa Abdalla, amedai katibu wa mamlaka ya KMA Nancy Karigithu, amekuwa na upendeleo katika kutoa ruzuku hiyo ya masomo kwa mabaharia.

Abdalla amesema kunafaa kuwe na usawa serikalini kuhusu maswala ya masomo ya mabaharia kwa kuwa ni kiungo muhimu katika uchumi na utendakazi wa taifa.

Amesema mabaharia wengi wa kwa sasa hawana vyeti kwani vyeti vyao vishaisha muda wa matumizi ilhali mamlaka inaendelea kuwatenga mabaharia haswa wa Pwani na kuwasidia watu wengine.

Wanasema ukabila na upendeleo unashuhudiwa katika mamlaka hiyo ya KMA kwani hata sheria za uchaguzi wa mabaharia hazifutiliwi huku wakipendekeza Nancy Karigithu aondelewe madarakani.