KimataifaMakalaMombasaWorld

Wapwani watakiwa kushirikiana na serikali ili kumaliza itikadi kali nchini……

Balozi wa Uingereza nchini Kenya Jane Mariott ametoa wito kwa jamii ukanda wa Pwani kushirikiana na serikali ili kumaliza suala la itikadi kali nchini.

Akizungumza mjini Malindi kwenye halfa ya kufungua afisi za kutetea haki za kibinadam za HAKI AFRICA Mariott amesema jamii inafaa kuwa na imani na maafisa wa usalama endapo watakuwa na taharuki kuhusu visa hivyo.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mkurugenzi wa Haki Africa ukanda wa pwani Hussein Khalid anayesema kwa muda sasa eneo hilo limekuwa likitumiwa na magaidi kusajili vijana wanaojiunga na kundi hilo haramu.

Wakati uohuo jaji wa mahakama kuu mjini humo Reuben Nyakundi amewashauri wenyeji kujitokeza na kuripoti visa hivyo ili watatue masuala hayo kabla kuyafikisha mahakamani.