HabariSiasa

Vikao vya bunge kukusanya maoni kuhusu BBI vyaanza……

Vikao vya pamoja vya kamati ya bunge la kitaifa ya sheria na ile ya seneti kukusanya maoni kutoka kwa umma kuhusu mswada wa marekebisho ya katiba vimeanza leo hii.

Tayari makundi mbali mbali yamefika mbele ya kikao hicho kuwasilisha hoja zao.

Miongoni mwa waliowasilisha hoja ni watu wanaoishi na ulemavu na mashirika ya kijamii.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya kikao hicho, mwenyekiti wa muungano wa mashirika ya kijamii Steven Cheboi amewashauri wakenya wote kuunga mkono mpango mzima wa BBI akisema unalenga kusaidia kukabil changamoto zinazowakumba wakenya.