HabariMombasaSiasa

Wanawake wahimizwa kuwania nafasi za uongozi…

Changamoto imetolewa kwa viongozi wanawake kuchukua fursa ya mpango wa maridhiano wa BBI kutafuta nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022.

 

Mwanaharakati wa siasa mama Zamzam Mohammed, amesema uchaguzi mkuu ujao umetoa nafasi nyingi za uongozi hasa iwapo mpango wa BBI utapitishwa na kuanza kutekelezwa.

 

Mama Zamzam pia amehimiza wanawake wenye azma ya kugombea nafasi za uongozi na hawana stakabadhi hitajika za masomo, kuchukua fursa hii kujiunga na taasisi mbali mbali za elimu ili kupata vyeti htajika.

 

Amesema anaimani ripoti hiyo itapitishwa na bunge la kitaifa na vile vile wananchi, kutokana na manufaa ambayo yanajitokeza ndani ya ripoti hiyo.