HabariMombasa

Wanaotekeleza mauaji ya wazee Kwale wasakwa…

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeanzisha kampeni ya kuwasaka wanaotekeleza mauaji ya wazee kutokana na ongezeko la visa hivyo kuripotiwa katika baadhi ya maeneo ya kaunti hio.

 

Kulingana na kamishna wa kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amesema kuwa tayari maafisa wa usalama wametengwa kuchunguza visa hivyo huku ikibainika kuwa wengi wa wazee walio uwawa ni kutokana na mizozo ya ardhi kinyume na inavyotambulika kuwa tuhuma za uchawi.

 

 

Kanyiri akisikitishwa na jinsi vijana walivyokosa utu na kuwaangamiza wazee wao huku kisa cha juzi kuripotiwa kikiwa eneo bunge la Lungalunga.

 

Amewaonya vijana na wakaazi wanaotekeleza unyama huo kuwa atakayepatikana akitekeleza visa hivyo mkono wa sheria hautawasaza.

 

Haya yanajiri huku akiwataka vijana kujishughulisha ili kujitafutia riziki badala ya kutegemea Mali za wazazi.