AfyaHabariWorld

SERIKALI YAORODHESHA HOSPITALI ZITAKAZOPEANA CHANJO YA COVID 19.

Hospitali za umma na za kibinafsi 622 kote nchini zimeidhinishwa kama vituo vya chanjo ya Covid-19 kama juhudi za serikali kuwezesha wananchi wengi wapate chanjo hiyo.

Hapa pwani tukianza na kaunti ya Mombasa Chanjo hiyo itapatikana katika vituo tisa ambapo ni hospitali za Mvita, Likoni, Changamwe, Kisauni, na Nyali.

Kwale ina vituo saba vilivyoorodheshwa; Kilifi ina vituo 13 huku wakazi wa Tana River wataweza kupata chanjo hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Hola, Ngao, na hospitali za kata ndogo za Bura.

Lamu ina vituo vitatu vilivyoidhinishwa, sawa na Tana River wakati wale wa Taita Taveta watapata chanjo katika vituo sita.