AfyaHabari

RAILA ATOKA HOSPITALINI.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu kuambukizwa Covid-19.

Katika kanda iliyochapishwa kwenye mtandao wake wa kijamii, Raila anaonekana akifanya mazoezi mepesi nje ya nyumba yake.

Raila amesikika akisema anafurahia sana kurejea  nyumbani na bado amejitenga hadi apate nafuu.

Raila alipelekwa hospitalini usiku wa Jumanne baada ya kuhisi uchovu  na maumivu.

Siku ya alhamisi jioni Raila alifichua kwa umma kuhusu hali yake ya kiafya na kutangaza hadharani kuwa alikuwa ameambukizwa virusi vya corona.