HabariKimataifa

Kenya yajiondoa kwenye kesi ya mpaka na Somalia.

Kenya imejiondoa katika kesi inayohusu mpaka kati yake na Somalia saa chache kabla ya kikao cha kusikilizwa kwa kesi hiyo katika mahakama ya kumataifa kuhusu uhalifu wa jinai ICC nchini Uholanzi.

Kwa sasa serikali inatarajiwa kuwasilisha rasmi notisi ya kujiondoa kwenye kesi hiyo ambayo inatarajiwa kusikiliswa asubuhi ya jumatatu hii.

Mnamo tarehe 9 mwezi machi mwaka huu wa 2021 mahakama ya ICC ilitangaza kuwa ingeongoza kesi kuhusu mzozo wa bahari hindi kati ya nchi hizo mbili ambazo ni Kenya na Somalia.