Habari

WANAFUNZO WAKOROFI WAONYWA KILIFI.

Idara ya usalama kaunti ya Kilifi imeonya wanafunzi watakaojihusisha na visa vya kuteketeza majengo ya shule.

Myenyekiti wa kamati ya usalama kaunti hiyo Kutswa Olaka anasema shule kadhaa hususan za malazi zimeteketezwa na wanafunzi na kusababisha hasara.

Olaka ameongeza kuwa mwanafunzi yeyote atakayejihusisha na visa vya kuteketeza moto mabweni kilifi atachukuliwa hatua kali za kisheria.