BurudaniEntertainmentHabari

Mwanamziki Christian Longomba Wa Longomba’s aaga dunia.

Tasnia ya mziki nchini Kenya imepata pigo baada ya mmoja wa waasisi wa mziki wa kizazi kipya inchini Kenya Christian Longomba wa Kundi maarufu Longomba’s ameaga dunia.

Christian Longomba aliaga dunia siku ya Jumamosi baada ya kuugua uvimbe wa ubongo.

Kupitia mtandao wa Kijamii ndugu yake Christian Longomba, Lovy Longomba alifunguka na kusema

‘KUKOSEKANA KWA MWILI NI KUWEPO NA BWANA.
NAKUPENDA NDUGU YANGU, RAFIKI YANGU NA MWENZANGU LAKINI YESU ANAKUPENDA ZAIDI. FURAHIA MBINGUNI. 

Logomba’s Wanafahimika sana kwa vibao vyao vilivyo tesa anga kama vile , vuta pumzi, piga makofi na queen.