Habari

Mwanamme ajitoa uhai Malindi.

Idara ya usalama kata ya Goshi,Wadi ya Kakuyuni eneo bunge la Malindi inachunguza kisa cha Mzee mmoja aliyejitia kitanzi nyumbani mwake katika mazingira tatanishi.

Kulingana na Mzee ya nyumba kumi wa Kijiji cha Kalatani  Elizabeth Zawadi Khamisi,Marehemu kwa jina Kahindi Karisa Kadenge amejitoa uhai baada ya kumtuma Bibi yake nje ya boma hilo ili atimize kisa hicho.

Kulingana na Zawadi, marehemu  amekuwa akisumbuliwa na msongo wa mawazo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya katika Hospitali kuu mjini Malindi.

Mzee wa Kijiji hicho, Nzaro Ngowa Tsuwi amedai Mzee huyo amechukua uamuzi huo baada ya madaktari kushauri familia iwe karibu naye kutokana na hali yake ya kiafya.

Kwa sasa mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Star mjini Malindi.

By Joseph yeri