AfyaHabari

Walimi kuanza kupokea chanjo ya covid 19.

Walimu nchini wanatazamiwa kuanza kupewa chanjo ya kukabili maambukizi ya virusi vya corona leo.

Walimu ni miongoni mwa waliopewa kupaumbele katika utoaji wa chanjo hiyo baada ya wahudumu wa afya kulingana na wizara ya afya nchini.

Chanjo hiyo inatolewa kwa walimu wanaotarajiwa kusimamia mitahani ya kitaifa ya KCSE na KCSE inayotarajiwa kuanza rasmi wiki ijayo.

Mwenyekiti wa jopo la kusimamia covid 19 Willis Akhwale amesema vituo vya kutoa chanjo hiyo vinatarajiwa kuongezeka na kufikia 575 kuanzia wiki hii hatua itakayoongeza idadi ya watu waliochajwa.

Kufikia wiki jana idadi ya watu waliochanjwa ilikuwa takriban elfu 10.

By News desk