HabariMombasa

Raia wa Tanzania akamatwa uwanja wa ndege Mombasa na Heroin.

Idara ya Polisi hapa Mjini Mombasa inasema inamzuilia mwanammke mmoja raia wa Tanzania aliyekamatwa jana jumapili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi Mombasa akiwa na dawa za kulevya aina ya Heroin.

Hii ni baada ya vitengo mbali mbali vya idara ya usalama kumkamata Maimuma Jumanne mwendo wa saa nane ambapo moja ya begi lake kupatikana na takriban kilo 5 ya dawa hizo.

Imebainika dawa hizo aina ya heroin zinathamani ya shilingi milioni 15.

Imearifiwa raia huyo mwenye cheti cha usafiri cha taifa la  Tanzania aliwasili kupitia ndege ya shirika la Ethiopia kutoka Johannesburg- Afrika Kusini, kupitia mji wa Addis Ababa, Ethiopia.