HabariNews

WANABODA MALINDI KUONGEZA NAULI.

Wahudumu wa Bodaboda mjini Malindi Kaunti ya Kilifi sasa wameapa kuongeza maradufu nauli kwa wateja wao baada ya kutangazwa ongezeko la bei ya mafuta ya Petroli kwa Shillingi saba zaidi humu Nchini.

Kulingana na Mwenyekiti wa wahudumu hao Kaunti ya Kilifi Joseph Mwangu tayari wamekubaliana na wahudumu wa bodaboda mjini humo kukutana juma hili ili kuafikiana kuhusu hatua hiyo.

Mwangu aanaitaka Serikali kutathmini upya bei ya bidhaa hiyo akidai ni hatua itakayokandamiza sekta hiyo na hata jamii kwa jumla.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na baadhi ya wahudumu hao mjini humo wakisema kwa sasa hawana budi ila kuongeza zaidi nauli kwa wateja wao.

Wanasisitiza haja ya Serikali kupunguza bei ya bidhaa hiyo ili kuwa afueni kwa sekta hiyo ambayo inategemewa na asilimia kubwa ya vijana Kaunti ya Kilifi.

By Joseph yeri