Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa serikali Cyrus Oguna aliyekuwa akizungumza na wanahabari wa hapa Mombasa.
Oguna ametetea hatua ya serikali kuendeleza uchunguzi wa abiria wanaotumia SGR hadi nyakati za usiku na kukosa kueka umbali unaohitajika ili kudhibiti maambukizi ya corona
Oguna ameshikilia kwamba ni jukumu la kila mwananchi kukataa kuabiri magari ya umma yasiyozingatia sheria zilizowekwa ili kujiepusha na athari za kuambukizwa ugonjwa huo ambao umeibuka upya .
Oguna aidha ametoa ushauri kwa washika dau katika sekta ya utalii pwani kufanya kila juhudi kuboresha utalii na kuongeza kua serikali imejizatiti kwa kubuni hazina maalum ya kuwasaidia wamiliki wa hoteli waliofilisika kutokana na janga la corona na kuanza upya.