HabariKimataifa

Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa Magufuli, huko Dodoma.

Maelfu ya raia wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli katika uwanja wa jamuhuri mjini Dodoma.

Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa nchi ambao wanahudhuria misa ya wafu ya hayati John Pombe Magufuli mjini Dodoma.

Rais Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki aliandamana na waziri Adan Mohammed.

Marais wengine wanaohudhuria ni pamoja na Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Lazaro Chakwera wa Malawi, Mokgweetsi Masisi wa Botswana.

Wengine ni Edgar Lungu wa Zambia, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Felix Tshisekedi wa DR Congo.

Marehemu Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli atazikwa Machi 26.

Leo mwili wake unatasalia katika uwanja wa Uhuru mjini Dodoma kwa uangalizi wa umma kabla ya kusafirishwa Mwanza Machi 23.

Siku hiyo hiyo, mwili utatasafirishwa katika mji alikozaliwa wa Chato ambapo wananchi watapata nafasi ya kuuona mwili huo.

Mnamo Machi 24, familia na wageni wote wa kimataifa na walioalikwa watapata nafasi kuutazama kabla ya siku ya mazishi.

Magufuli alifariki dunia mnamo Machi 17.