HabariKimataifa

Mwili wa Magufuli wawasili Zanzibar ili kuagwa rasmi….

Viongozi wa serikali na dini mbalimbali pamoja na wananchi tayari wamejitokeza katika viwanja vya Amani Karume Kisiwani Zanzibar kuaga mwili ya hayati John Pombe Magufuli.

Mwili wa Magufuli umewasili katika uwanja huo na zoezi la kuuaga litaanza rasmi likiongozwa na rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi.

kabla ya kufika kwenye uwanja huo wa Amani, msafara uliobeba mwili wake ulipitishwa kwenye maeneo mbalimbali ya mitaa ambapo wananchi walikuwa wamepiga safu barabarani wakiusubiri.

Hapo kesho mwili wa Magufuli utasafirishwa hadi Mwanza ili kuagwa na wananchi kabla ya kusafirishwa mkoani Chato na kuzikwa siku ya ijumaa.

Hapo jana marais 10 wa Afrika walihudhuria misa ya Magufuli katika uwanja wa Jamuhuri