AfyaHabariMombasa

Hospitali ya Jocham ni ya kwanza kutoa chanjo ya covid 19….

Hospitali ya kibinafsi ya Jocham hapa mjini Mombasa imekuwa ya kwanza miongoni mwa hospitali za kibinafsi kuanza kutoa chanjo ya kuthibiti maambukizi ya virusi vya covid-19.

Kulingana na daktari John Chami,utoji wa chanjo hiyo utaanza na wahudumu wa afya wakifuatiwa na waalimu na idara ya usalama huku shughuli hio ikiendelea baadae kwa wakenya wengine bila malipo.

Wakadi huo huo, Chami amewashahuri wakenya kutokuwa na hofu akisema chanjo hiyo ni salama.