AfyaHabari

Wanahabari wahimizwa kupimwa virusi vya corona…

Ushirika wa waandishi wa habari Ukanda wa Pwani sasa wanawataka wanahabari Nchini kutembelea taasisi za afya kupimwa virusi vya Corona.

Mshirikishi wa muungano huo Baya Kitsao, amesistiza haja ya wanahabari kufanya hivyo ili kuepeuka maambukizi ya virusi hivyo kwa wanahabari Zaidi.

Kauli ya Baya inajiri baada ya kubainika kwamba kumekuwa na ongezeko la maambukizi hayo miongoni mwa wanahabari Nchini na hata baadhi kupoteza maisha.

Wakati uo huo Baya amekiri kwamba kuhudhuria kwa mikusanyiko miongoni mwa wanahabari kutafuta habari kumewaweka wengi wao kuwa katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo na kwamba ipo haja ya kuwa makini hata Zaidi.