AfyaHabari

Maafisa wa usalama Taita Taveta washauriwa kupata chanjo wa CORONA…..

Maafisa wa usalama sawa na maafisa wa utawala wa mkoa kaunti ya Taita Taveta wameshauriwa kupata chanjo ya kujikinga kutokana na maambukizi ya Corona.

Akiongea baada ya kupokea chanjo hiyo katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi,kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Rhoda Onyancha anasema maafisa hao hutangamana moja kwa moja na wananchi na itakua vyema iwapo wataanza kupokea chanjo hiyo.

Onyancha aidha amewataka wananchi kuzingatia maagizo ya wizara ya afya ya kukabili kusambaa kwa virusi hivyo kwani wengi wamekuwa wakipuuza.

Kwa upande wake kamanda wa mkuu wa polisi kaunti ya Taita Taveta Patrick Okeri anasema kwamba maafisa wa usalama wataendelea na msako wa kuwakamata wanaopuuza masharti ya wizara ya afya.