Ripoti ya wizara ya afya kuhusu hali ya chanjo humu nchini inaonyesha kwamba kufikia leo jumla ya watu waliopata chanjo ni elfu 422,628.
Ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu shughuli ya utoaji chanjo kuzinduliwa rasmi, watu elfu 422,400 wamepata chanjo hiyo ya Astrazeneca,huku wengine 228 wakipata chanjo ya Sputnik V.
Kulingana na ripoti hiyo, miongoni mwa idadi, jumla ya watu waliochanjwa, wanaume asilimia 56.5 wamechanjwa huku asilimia 43.5 ya wanawake wakipata chanjo hiyo.
kaunti ya Nairobi inaongoza kwa idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kuchanjwa huku Lamu ikiwa na idadi ndogo zaidi ya wanaojitokeza kuchanjwa.
Katika kaunti ya Uasin Gishu, watu 21,382 wamepewa chanjo, 19,432 huko Kiambu, Kisumu 14,337, Nyeri 12,774, Kajiado 12,553, Mombasa 10,977, Kakamega 10,337, na Muranga 9,778.
aidha ripoti hiyo imeweka wazi changamoto zinazosababisha idadi ndogo ya watu wanaochanjwa ambao ni kucheleweshwa kwa kujazwa kwa ripoti katika mtandao wa chanjo.ke , kufuatia uhaba wa vifaa katika mitandao pamoja na umati mkubwa wa watu wanaotafuta huduma hiyo.