Habari

Kenya na Tanzania zimebuni kamati ya ushirikiano…………………………………..

Rais wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan ameagiza kubuniwa kwa kamati hio leo hii wakati alipoufanya mkutano na waziri wa michezo wa Kenya Amina Mohammed aliyemwakilisha Rais Uhuru Kenyatta.

Amina ambaye ameandamana na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amewasilisha ujumbe wa Rais Kenyatta ambaye ameahidi kushirikiana na taifa hilo jirani kwa manufaa ya Raia .

Rais Samia kwa upande wake ameahidi kuendeleza urafiki baina ya Kenya na Tanzania ambao uliodumishwa na mwendazake Rais Pombe Magufuli.

Aidha amesema atashughulikia tofauti zote zilizoko baina ya mataifa  haya mawili. Huu ni ujumbe wa kwanza kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta tangu Rais Samia kuingia madarakani wiki chache zilizopita kufuatia kifo cha Magufuli huku wakimkaribisha kufanya ziara nchini.