Habari

Mahojiano ya waliotuma maombi kujaza nafasi ya Jaji Mkuu yataanza rasmi siku ya Jumatatu………………….

Tume ya huduma za mahakama JSC zimethibitisha kwamba mahojiano ya waliotuma maombi kujaza nafasi ya Jaji Mkuu yataanza rasmi siku ya Jumatatu.

kupitia mtandao wake Twitter JSC imesema kwamba shughuli hiyo itafanyika katika majengo ya mahakama ya juu na pia kupeperushwa kupitia wavuti wake rasmi.

JSC ilipokea majina ya watu 13 wanaotaka kumrithi David Maraga aliyestaafu mapema mwaka huu huku 10 pekee yakiidhinishwa.

wakwanza kuhojiwa atakuwa Jaji Kitembwe Said Juma atakayefika mbele ya Tume hiyo Jumatatu saa Tatu asubui.