Habari

Mwili wa mwanamke uliokatwa katwa wapatikana huko KESE, Wundanyi…..

Wakaazi wa Kijiji cha Werugha Kese eneo bunge la Wundanyi Kaunti ya Taita Taveta,wameamkia kisa cha kushangaza ambapo mwili wa mwanamke umepatikana katika eneo hilo ukiwa umekatwa sehemu kadha za mwili ikiwemo ,kichwa,mikono na miguu.

Paul Mtoto ni mmoja wa walioshudia kisa hicho.

Akidhibitisha kisa hicho naibu chifu wa Werugha Christina Mwanaisha Kidago,amesema kwamba huenda mwili huo ulitwaliwa kutoka sehemu nyingine na kutupwa eneo hilo,baada ya mwanamke mwendazake kufanyiwa unyama huo.

Aidha ,naibu huyo wa chifu amesema tayari mafisa wa usalama wamefika katika eneo la tukio na uchunguzi tayari umeanzishwa kubaini kilichopelekea mauwaji hayo.