Habari

Proffesa Patricia Mbote ahojiwa kwa wadhfa wa jaji mkuu……

Mahoajiano ya kujaza wadhfa wa jaji mkuu yanaendelea kwa sasa ambapo leo anahojiwa proffesa Patricia Kameri Mbote, ambapo amesema iwapo ataidhinishwa kuwa jaji mkuu na pia mwenyekiti wa tume ya huduma za mahakama, jukumu lake kubwa litakuwa ni kuhakikisha kwamba kuna rasilimali za kutosha kufanikisha huduma katika tume hiyo.

Akihojiwa, Mbote amesema kulingana na uchunguzi aliofanya, changamoto ya kifedha ni moja wapo ya masuala ambayo yameathiri utendakazi katika idara ya mahakama.

Proffesa Mbote amesema iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu atahakikisha kuwa maamuzi yanayofanywa na mahakama ya juu yanakuwa ya haki na ambayo yanazingatia sheria.

Jaji wa mahakama ya rufaa Mohammed Warsame pia alimtaka kufafanua vipi atashughulikia suala la amri za mahakama kukiukwa na hata kutofuatwa.

kuhusu hatua ya rais Uhuru Kenyatta ya kukataa kuwaidhinisha majaji 41 waliopendekezwa na tume ya huduma za mahakama, katika jibu lake, Mbote amesema iwapo atachaguliwa kuwa jaji mkuu atamfuata rais Kenyatta yeye binafsi na kumuhimizi kuwaidhinisha majaji hao.