HabariMombasa

Waislamu Mombasa wako mbioni kukamilisha matayarisho ya ramadhan…

Waumini wa dini ya kiislamu hapa mjini Mombasa leo wamejitokeza katika soko la Marikiti kwa shughuli za kununua bidhaa kwa maandalizi ya mwezi mtukufu wa Ramadan uliotangazwa kuanza hapo kesho.

Baadhi ya waumini hao wanasema hali ya uchumi imedorora kufuatia janga la corona huku wengine wakilalamikia bei ya juu ya baadhi ya bidhaa.

Aidha wauzaji kwenye soko hilo la marikiti wamelalamikia idadi ndogo ya wateja ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Hapo jana kadhi mkuu wa Kenya Shariff Ahmed Muhdhar alitangaza kwamba ramadhan itaanza hapo kesho jumatano baada ya mwezi kutoonekana katika mataifa ya Afrika Mashariki.