Serikali ya kaunti ya Kilifi imeweka mikakati kabambe ya kuimarisha soko kuu la Gongoni ili kuwawezesha wafanyibiashara sokoni humu kuendeleza shughuli zao katika mazingira bora.
Kulingana na Mwakilishi wa Wadi ya Gongoni Albert Kiraga tayari serikali ya kaunti imeanza kuunganisha soko hilo na maji, nguvu za umeme pamoja na vyumba vya kutosha kwa wafanyibiashara.
Akizungumza na kitu hiki Kiraga amebainisha kuwa serikali hiyo imetumia takriban Shillingi million 58 katika kuwekeza mradi wa soko hilo huku akidokeza kuwa wanalenga kulifanya kuwa kitovu cha biashara kwa wakaazi wa Malindi na Magarini.
Wakati uohuo Kiraga amesema kuwa baadhi ya miradi ya serikali ya kaunti iliyokuwa imeanza kutekelezwa kwa sasa imesimamishwa eneo hilo kutokana na mvua inayoendelea kunyesha.
Kiraga sasa amewataka wakaazi wa eneo lake la uwakalishi kuwa na subra,akisisitiza miradi ya barabara iliyozinduliwa hivi majuzi itaendelezwa kutakapokuwa na kiangazi