Habari

Ukur Yattani akosa kufika mbele ya kamati za bunge…

Waziri wa fedha Ukur Yatani amedinda kufika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu fedha kuzungumzia suala la deni ambalo Kenya imechukua kutoka kwa shirika la fedha duniani IMF na mashirika mengine ya kimataifa.

Deni hilo la IMF la shilingi bilioni 255 limeibua hisia kutoka kwa wakenya huku wengi wakilalamikia hulka ya Kenya kuendelea kuchukua deni linalozidi kuwa mzigo mkubwa kwa wakenya.

Yattani  alikuwa afike mbele ya kamati hio iliyoongozwa na mwakilishi wa kina mama kaunti ya Homa Bay Gladys Wanga mapema leo ingawa mkutano huo ulifutuliwa mbali akieleza kamati hiyo alikuwa na shughuli zingine na hivyo hangeweza kufika mbele ya wabunge hao.