Vijana wa Lamu wameanzisha bunge la vijana la kaunti ya Lamu linalolenga kuangazia changamoto zinazowakabili hasa suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ili wapate kuzitatua kupitia serikali zote mbili.
Bunge hilo limefanya kikao chake cha kwanza katika jengo la bunge la zamani la kaunti ya Lamu kisiwani Amu, na kujadili mswada wa Blue Economy ili kuona ni vipi vijana wa Lamu watanufaika na kazi za baharini ikiwemo bandari ya Lamu.
Aidha bunge la vijana linahusisha watu zaidi ya 30 miongoni mwao Rais wa vijana ambaye ni mwenyekiti wa bunge naibu wa Rais spika na mawaziri 10 sawa na wabunge 25 waliochaguliwa na walioteuliwa.