Habari

Mumo Faith Kamwi kutoka shule ya Kari Mwailu ndiye mwanafunzi bora zaidi katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE bada ya kupata alama 433.

Mwanafunzi wa pili ni msichana Wesonga Nanzala kutoka  shule ya wasichana ya Chogoria akiwa na alam 432 akiwa sawa na Murithi Angle kutoka shule ya msingi ya Maseno.

Nafasai ya 10 bora ikichukulwa na Samuel Wanyonyi 431, Castro William 431, Maureen Tarus 431, Abiud Kipkurui 430, Margaret Mwangi 430, Dennis Omondi 429, Joyce Nkatha 429.

Akitangaza matokeo hayo katika jumba la mtihani house jijini Nairobi,Waziri wa Elimu nchini Prof George Magoha amesema wanafunzi wakike ndio waliongoza kwa wingi katika mtihani huo wakiwa 8 kati ya 15 wa kwanza.

Shule za umma pia zimefanya vyema mwaka huu kukiwa na shule 10 za umma ati ya shule 15 zinazoongoza.

akihojiwa na kituo kimoja cha habarai mwanafunzi huyo bingwa Mumo Faith Makwi,ameelezea hisia zake kuhusiana na matokeo hayo.

matokeo bora yalirekodiwa katika msomo matano ikilinganishwa na mwaka ulipota,yakiwemo,Hisabati,insha ya kiingereza,matokeo duni yakirekodiwa kiingereza Kiswahili mioongoni mwa mengine.

Wakati huo huo waziri huyo amesema kwamba matokeo hayo hayana tofauti kubwa ikilinganishw a na mitiani iliyofanywa hapo akiwashukuru waalimu kwa kujitolea kwa hali na mali kuhakikikisha kwamba zoezi hilo linafanyika bila kutatizika.

Wakati huohuo waziri Magoha ametangaza kuwa watahiniwa wote waliofaya mtihani huo watajiunga na shule za upili kufuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta huku wale waliojihusisha na udanganyifu watakabiliwa na sheria.

Waziri magoha ameongeza kuwa teuzi wa wanafunzi kwenda shule mbalimbali unatarajiwa kuanza rasmi mwezi ujao tayai kwa wanafunzi hao kujiunga na shule za upili.

jumla ya wanafunzi 1,179, 191 wamekalia mtihani wao wakcpe mwaka huu.