Habari

Wanafunzi wa KCPE watakaopata alama ya 300 na zaidi Lamu kusomeshwa bure…

Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Twaha amewahakikishia wanafunzi wote wa lamu  waliofanya mtihani wa KCPE ambao watajizolea alama 300 na zaidi wataendeleza masomo yao bila ya kulipa karo shuleni.

Twaha amesema kuwa kaunti ya Lamu itawafadhili kikamilifu wanafunzi ambao watajizolea alama 300 na zaidi na kwamba wazazi wanatakiwa kununua vitabu, sare za shule na vifaa vinginevyo vya shule.

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi, gavana Twaha amesema kwamba wanafunzi wataokamilisha kidato ncha nne serikali ya kitaifa itawapa mikopo ya kujiendeleza kielimu maarufu HELB.