HabariSiasa

Ngatia asema kesi za uchaguzi wa urais ziendelea kusikizwa na mahakama ya juu….

Wakili Fredrick Ngatia ambaye anahojiwa kwenye mahojiano ya kumtafuta jaji mkuu ametakiwa kueleza maswala matatu ambayo anahisi ni changamoto katika idara ya mahakama na jinsi atatekeleza utenda kazi wake kuhakikisha kuwa idara ya mahakama inakuwa kwa kiwango kingine.

Ngatia amesema kuwa tatizo kubwa ambalo limekuwepo kwa muda ni jinsi kesi zinavyosikizwa na jinsi maamuzi yanavyotolewa mahakamani.

Akiendelea kuhojiwa Ngatia ameeleza umuhimu wa kesi kuhusu uchaguzi wa urais kuendelea kusikizwa na mahakama ya juu.

Akijibu swali la naibu jaji Mkuu Philomena Mwilu kuhusu mahakama inayopaswa kusikiza kesi hizo, Ngatia amesema iwapo kesi za urais zitasikizwa na mahakama ya chini zitachangia uwepo wa rufaa nyingi na kuchelewa kutolewa kwa maamuzi.

Wakati huo huo wakili Ngatia ametakiwa kufafanua kuhusu muda ambao unatakikana katika kusikiliza kesi ya urais kwani ilivyo kwa sasa muda huo ni siku 14, Ngatia akisema cha muhimu ni kuzipatia pande zinazohusika muda wa kuwasilisha hoja zake mahakamani ili haki ipatikane.