HabariLifestyle

Raila aeleza masikitiko kufuatia ongezeko la mauaji ya wanandoa…..

Kinara wa ODM Raila Odinga amelalamikia ongezeko la visa vya mauaji baina ya wanandoa kufuatia mizozo ya kifamilia humu nchini.

Ansema kulingana na ripoti kutoka kwa vyombo vya habari, ni wazi kwamba watu wengi wanaendelea kupoteza maisha yao kufuatia mizozo ya kinyumbani.

Kupitia taarifa yake, Raila ameshinikiza kuwepo kwa mjadala wa kitaifa kuhusu athari ya mizozo ya kijinsia katika familia ili kuweza kuzuia maafa na hata vifo zaidi.

Ameshauri iwapo mwanandoa atakuwa hawezi tena kuvumilia kwenye ndoa hiyo ni bora kutalakiana badala ya kusubiri na kisha kuuliwa.

Kauli yake inajiri huku visa vya wapenzi kuuwana vikiongezeka.

Hivi majuzi huko Mbooni Mashariki, mwanamume mmoja alimkatakata mkewe hadi kufa juu ya mzozo wa ardhi. na kisha baadae aliuawa na wanakijiji waliokuwa na hasira.

Mnamo Aprili 8, mwanamume mmoja alimuua mkewe mjamzito na watoto wawili kwa kutumia nyundo katika eneo la Mbeere Kusini.