Habari

Profesa Dkt Moni Wekesa atatizika kujibu maswali ya jopo la JSC…….

Profesa Dkt Moni Wekesa ambaye anahojiwa na tume ya huduma za mahakama JSC katika mahojiano ya kumtafuta jaji mkuu amepitwa na maswali kadhaa aliyoulizwa na kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu kuhusu mbinu za uongozi ambazo anapania kutumia katika kuboresha utendakazi wa idara ya mahakama.

Aidha Wekesa amesema iwapo ataidhinishwa kuwa jaji mkuu atahakikisha mipango ya idara ya mahakama inafanikishwa kwa kupitia vipindi kwenye vyombo vya habari tofauti na ilivyo kwa sasa habari muhimu za idara hiyo zitawafikia wakenya kupitia vipindi kama vya runinga.

Wekesa aidha amesema kwamba mojawapo ya ajenda  zake ni kuhakikisha wakenya wanaelewa mfumo wa utendakazi wa mahakama kwa kuwahamasisha ili kuondoa dhana kwamba maamuzi yake yanachochewa na ufisadi miongoni mwa maafisa wake.

Profesa Wekesa ni muaniaji wa tisa kuhojiwa ambapo mauniaji wa mwisho atahojiwa hapo kesho.

 

By News Desk