Wakazi wa kijiji cha Magorani wadi ya Tezo kaunti ya Kilifi wameelezea masaibu wanayopitia wanapopatwa na lazima ya kwenda haja kubwa kutokana na ukosefu wa vyoo vya umma eneo hilo.
Kulingana na wakaazi hao wameendelea kutaabika kwa muda mrefu na kulazimika kuenda misituni kujisaidia
Wakiongozwa na Roseline Migoti wanasema gharama za kuchimba vyoo ni ghali zaidi kutokana na sehemu hiyo kuwa na mawe, na sasa wanaitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuwajengea vyoo ili kuwaondolea masaibu hayo.
Mwanaharakati wa mazingira na afya wadi ya Tezo Beatrice Mwinga, anasema afueni itapatikana iwapo serikali itawajengea wakazi na wafanyibiashara vyoo eneo hilo.
Ameeleza hofu yake kuwa huenda mkurupuko wa maradhi tofauti tofauti ikiwemo kipindupindu ukashuhudiwa eneo hilo kutokana na ukosefu wa vyoo.
By: News Desk