Wawakilishi wadi wa wanawake kaunti ya Taita Taveta wamejitokeza na kusema watatoa hamasa kuhusu athari za ukeketaji miongoni mwa watoto wadogo kaunti hiyo.
Wameongezea kuwa wakati wa likizo watoto wadogo na wasichana ndio walengwa kuu wa ukeketaji huku akitoa wito wa ushirikiano baina ya taasisi mbalimbali za serikali na jamii.
Wakiongozwa na Joyce Mwangoji wamesema kuwa sharti jamii ihamasishwe vilivyo kuhusu athari za ukeketaji.
Aidha wawakilishi hao wamesema kuna haja ya maafisa wa utawala wa mkuu hasa machifu kuhusika kikamilifu kupinga ukeketaji kwani wako nyanjani mara kwa mara.
Haya yanajiri huku baraza la wazee kaunti hiyo likiunga mkono kampeni hiyo ya kukomesha ukeketaji wanaoitaja kama mila iliyopitwa na wakti.
By News Desk