Mkurugenzi wa halmashauri ya usimamizi wa shughuli za usafirishaji (KMA) kaunti ya lamu Alex Munga, amewasihi wakaazi wa lamu kuchukua tahadhari, kutokana na uwezekano wa upepo mkali na mafuriko unaotarajiwa baharini kutokana na kimbunga.
Munga amewasihi watumizi wa vyombo vya baharini na wavuvi wote kuwa makini na kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa zote zitakazokuwa zinatolewana na halmashauri hiyo endapo hali itabadilika kiasi cha kuhatarisha usalama baharini
Aidha wakaazi wa lamu wametakiwa kukatiza safari za visiwani zisizokua na ulazima ili kuepuka majanga ambayo huenda yakashuhudiwa.