HabariSiasa

Vikao vya kujadili mswada wa BBI vyaendelea bungeni……….

Mwenyekiti wa kamati ya pamoja inayoshughulikia mswada wa marekbisho ya katiba wa mwaka 2020 seneta Okongo Omogeni amelihimiza bunge la seneti kufanyia marekibisho sehemu zinazoibua utata katika mswada huo.

Akiwasilisha hoja zake wakati wa kikao cha kujadili mswada huo, Omogen amesema sehemu zinazopaswa kufanyiwa marekeisho ni zile zilizo na makosa madogo madogo ambazo haziwezi kuathiri uhalisia wa mswada wa  BBI.

Ameliomba bunge la seneti kuafikiana kwa kauli moja na kuidhinisha marekebisho kadhaa ya mswada huo kabla ya kuwasalisha kwa wakenya kupiga kura ya kuunga au kuupinga.

Aidha Omogeni ametumia fursa hiyo kufafanua sehemu za mswada ambazo kamati yake ilizifanyia marekebisho.

Omogeni ametaja kipengele cha uteuzi wa majaji vilevile makamishna wanaopaswa kuwahoji majaji wakati maadili yao yanapotiliwa shaka.

Vilevile ametaja vipengee vya ugavi wa rasilimali na utendakazi wa tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC kuwa miongoni mwa walivyovipiga msasa.

Seneta wa Murang’a Irungu Kangata aidha ameendelea kuukosoa mswada huo akisema haelewi mfumo uliotumika kubuniwa na kugawanywa kwa maeneo bunge.

Kulingana naye eneo la Mlima Kenya ambalo lina idadi kubwa ya watu halijanufaika na maeneo yao ilhali maeneo ya Pwani yalipata maeneo mapya kati ya sabini yaliyobuniwa

Mjadala sawa na huo unaendelea katika bunge la kitaifa huku mbunge wa Rarieda Otiende Amollo akitetea hatua ya kamati ya pamoja ya sheria na haki JLAK kuweka wazi baadhi ya maswala yenye utata katika mswaad awa BBI.

Amollo ambaye alikuwa mwanachama wa kamati hiyo amesema kwamba hali hiyo ililenga kutoa mwanga kuhusu yaliyopo katika mswada ili kuwapa wananchi fursa yakufanya uamuzi wa busara katika kura ya maamuzi

By: Reporter Joyce Mwendwa