Baadhi ya wakimbizi wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kwenye Kaunti ya Turkana wamekerwa na mipango ya Serikali kusema kwamba Kambi hiyo itafungwa ifikapo mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Wakimbizi hao aidha wanadai kwamba migogoro katika Mataifa yao iliyowasababisha watoroke bado wanaendelea hivyo hatua ya kuwataka kurejea inahatarisha maisha yao.
Wakimbizi hao wamependekeza kupelekwa katika Mataifa mengine yenye usalama badala ya kurejeshwa Nchini mwao.
Hizi hapa hisia za baadhi ya wakimbizi hao.
Kilio chao kinajiri siku moja baada ya Serikali kuafikiana na Shirika La Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UNHCR kufunga kambi za wakimbizi za Baadab na Kakuma ifikapo Juni mwaka ujao.
Itakumbukwa kwamba Kenya na UNHCR ziliafikiana kuhusu masuala muhimu yanayostahili kutekelezwa kabla ya kambi hizo kufungwa, katika maafikiano hayo ni kwamba Kenya ifanikishe kuwarejesha katika Nchi zao wakimbizi hao kwa hiari na kwa usalama.
Na wasioweza kurejea kutokana na sababu mbali mbali, Kenya iweke mipango ya kuwawezesha kwenda kuishi katika mataifa mengine, na wakimbizi ambao ni raia wa mataifa ya Afrika ya Mashariki kuruhusiwa katika sehemu nyengine Nchini.
UNHCR aidha inataka Kenya kuwapatia vitambulisha vya kitaifa Wakenya elfu 11 waliojisajili kuwa wakimbizi kwa lengo la kupata misaada.