AfyaHabariMombasa

Chanjo ya Astrazeneca iliyosalia Mombasa ni kidogo mno….

Idadi ya chanjo ya Astrazeneca ambayo imesalia katika kaunti ya Mombasa imebainika kwamba haitakidhi mahitaji ya watu ambao wamesajiliwa na wanasubiri chanjo hiyo.

Kufikia sasa jumla ya watu 3,137 wamesajiliwa kupewa chanjo iliyosalia huku chanjo iliyosalia ikiwa ni elfu 1,438 pekee.

hii inamaanisha kwamba jumla ya watu 1,696 ambao hawajapata fursa ya kuchanjwa watasubiri hadi wakati ambapo chanjo ya kampuni ya Fizer na Johnson and Johnson zitakapowasili nchini.

Kaunti ya Mombasa ilipokea jumla ya chanjo elfu 24 kutoka wizara ya afya na kufikia sasa jumla ya chanjo 22,500 zimetolewa.

Ikumbukwe kwamba wiki moja iliyopita waziri wa afya Mutahi Kagwe alikiri kuwepo kwa uhaba wa chanjo ya Astrazeneca kufuatia changamoto inayokabili taasisi ya serum nchini India inayotengeneza chanjo hiyo.

By Reporter Warda Ahmed