Rais Uhuru Kenyatta amemtaka waziri wa Kilimo nchini Peter Munya kuondoa marufuku ya uagizaji wa mahindi kutoka Uganda na Tanzania.
Agizo hili limetolewa kufuatia hatua ya kuondoa vizuizi vya kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais Kenyatta akiwahimiza mawaziri toka mataifa yote mawili kufanya kazi kwa pamoja
Rais Kenyatta aidha ametaka upimwaji wa virusi vya corona katika border za Tanzania kuharakishwa ili kupunguza msongamano wa magari.
By NewsDesk